HabariLifestyleNews

WACHUUZI KUHAMIA SOKO JIPYA LA MVINDENI KAUNTI YA KWALE.

Zaidi ya wachuuzi 500 wa sokoni  katika eneo la Diani kaunti ya Kwale wameanza kuhamia katika soko jipya la Mvindeni.

Soko hilo lililokarabatiwa na serikali ya kaunti hiyo baada ya soko la Ibiza kubomolewa mnamo mwaka 2018 kupisha upanuzi wa barabara.

Akielezea furaha yake Catherine Robert ambaye ni mchuuzi katika soko la Ibiza amesema kuwa kuhamia katika soko hilo jipya la Mvindeni sasa kutampuzisha mahangaiko aliyokuwa akipitia tangu mwaka 2018.

Sawia na David Murigi ambaye ni mchuuzi wa tomato akititaka serikali ya kaunti ya Kwale kuharakisha kukamilisha ujenzi kwenye soko hilo.

Wachuuzi hao wakisemakuwa maisha yamekuwa magumu kwao kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha hapa nchini.

Mary Ayuma ambaye ni mchuuzi akisema kuwa mara nyingi wakihangaika kutafuta mahali pa kununua vyakula kwani hakukuwa na soko maalum.

Huku Edna Sabina akisemakuwa kama wachuuzi wanatarajia kuwa biashara zao zitakuwa salama kutokana na ukuta uliozungushwa katika soko hilo jipya.

BY NEWS DESK