HabariLifestyleMombasaNews

WANAKANDARASI KAUNTI YA KWALE WAAGIZWA KUZINGATIA WENYEJI WAKATI WA KUTOA AJIRA.

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewaagiza wanakandarasi wanaosimamia miradi ya maendeleo ya Kaunti wawapatie kipaumbele katika utoaji nafasi za ajira wenyeji wa maeneo kunakofanyika miradi hiyo.

Akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi ya ujenzi wa shule za chekechea za Ganda huko Pongwe/Kikoneni na ile ya Kiduka wadi ya Vanga Bi. Achani aidha amewataka wanakandarasi wazingatie ubora wa ujenzi katika miradi hiyo ya umma.

Wakati uo huo amewahimiza wananchi wajiepushe na siasa, na washirikiane na usimamizi wa Serikali ya Kaunti kwa ajili ya kufanikisha ajenda za maendeleo.

Kwa upande wao wakazi wa maeneo hayo wameipongeza Serikali ya Kaunti ya Kwale kwa kuwafikishia miradi ya maendeleo mashinani.

Guni Bati ni mwenyeji wa kijiji cha Ganda.

 

BY NEWS DESK