Timu ya kitaifa ya kandanda nchini, Harambee stars iliwasili jijini Doha Qatar kujitayarisha kwa mechi dhidi ya Qatar katika uga wa Al Janoub Alhamisi Septemba 7, 2023.Wachezaji sita pekee wanaochezea vilabu nchini Kenya ndio walioteuliwa katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa na kocha mkuu Engin Firat.Miongoni mwa walioteuliwa ni;
Walinda lango: Ian Otieno kutoka Zesco, Zambia, Byrne Odhiambo wa KCB, Patrick Matasi kutoka Kenya Police FC.
Safu ya Ulinzi: Collins Sichenje wa AIK, Swiden, Joseph Okumu kutoka state Reims, Ufanansa , Brian Mandela akichezea Mamelodi Sundowns, South Africa , Johnstone Omurwa wa Estrela, Portugal , Daniel Anyembe kutoka Viborg, Denmark, Eric Ouma akichezea AIK, Sweden , Amos Nondi akigaragara soka Ararat, Armenia, Abud Omar wa Kenya Police fc.
Safu ya kati: Richard Odada (AaB, Denmark), Teddy Akumu (Sagan)Tosu, Japan), Kenneth Muguna (Kenya Police), Timothy Ouma (IF Elfsborg, Sweden), Duke Abuya (Singida Fountain Gate, Tanzania), Ayub Masika (Nanjing City Football Club, China), Alfred Scriven (IL Hødd, Norway), Clarke Oduor (Bradford City AFC, England).
Washambulizi : Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Elvis Rupia (Kenya Police), Michael Olunga (Al Duhail, Qatar), Masud Juma (Al Jabalain, Saudi Arabia)
Hata hivyo timu hiyo inatarajiwa kuregea nchini Ijumaa kuendelea na matayarisho yake dhidi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan Kusini siku ya Jumanne Septemba 12, 2023.