HabariNews

Serikali ihamasishe walemavu kuhusu mahitajio ya usajili wa Inua Jamii

Serikali imehimizwa kuihamasisha jamii hasa ya watu wanaoishi na ulemavu kuhusu mahitaji ya kusajiliwa kwa walengwa wa mpango wa Inua Jamii.

Kulingana na Josephat Musungu, Mwenyekiti wa Shirika la Watu Wanaoishi na Ulemavu wa Ngozi kaunti ya Mombasa walemavu wengi nchini hawafahamu mahitaji stahiki yaliowekwa na serikali katika kuwasajili na kuwajumuisha kama walengwa wa fedha za mpango wa inua jami.

Aidha aliitaka serikali kulegeza sheria walizowekwa kwenye mchakato wa kuendesha zoezi hilo kwa kubuni sera na shereia zitakazoweza kuwafaidisha wengi na mpango huo.

“Serikali haijafanya hamasa kwa watu wanaoishi na ulemavu wajue ni walemavu gani wanaofaa kusajiliwa kwa sababu ni wale walemavu ambao wako chini ya uangalizi masaa 24 ndio wanaolengwa kwa sasa.serikali ikuje na mpango mwengine pia iweze kupanua mpango huo ili kuzingatia mtu ambaye ni mlemavu na hana kazi.” Alisema Musungu.

Wakati huo huo alitoa ombi kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kushirikiana na ile ya kitaifa kukarabati majengo yenye ofisi za serikali kwa kuwawekea njia maalum ili kuwawezesha watu wanaoishi na ulemavu kupata huduma hizo bila vikwazo.

“Mlemavu kupanda kule juu kwa gallery ya bunge la kaunti, jengo la Bima tower na Betting control ni ngumu kwa hiyo tunamuomba gavana na serikali ya kitaifa kukaa chini na kujua tatizo lipo wapi na kuja na suluhu.” Alikariri Musungu.

BY BEBI SHEMAWIA