HabariNews

Mradi wa Nyumba za Kisasa wazinduliwa Kisauni; Zaidi ya Vijana 2,000 kunufaika na nafasi za Ajira

Vijana eneobunge la Kisauni wanatarajiwa kunufaika na nafasi za ajira kutokana na mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za Santana.

Mradi huo chini ya kampuni ya ujenzi ya Megna Homes umezinduliwa rasmi katika eneo la Mtopanga eneobunge la Kisauni ukitarajiwa kuajiri zaidi ya vijana 2,000.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo Ahmed Badawy amesema ujenzi huo wa makazi ya kifahari SANTANA utakaokuwa na nyumba  zaidi 816  utaboresha usalama, ukuaji wa kiuchumi na kukuza talanta miongoni mwa vijana na kutaka jamii kutoka eneo hilo kukumbatia mpango huo.

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na Afisa Mkuu Mtendaji wa Megna Homes Ahmed Badawy

“Hapa Kisauni tunekuwa na utata mwingi wa insecurity lakini sasa mradi huu unakuja na kituo cha polisi hapa. Nyumba zitakuwa gated community; na jambo la ajira limekuwa tatizo hapa Kisauni lakini kupitia mradi huu kutapatikana kazi zaidi ya 2,000 mbali na uwanja wa michezo wa seven aside.

Na hata mradi ukiisha zile za ujenzi, kazi zote zitakazopatikana hapa zitakuwa kwa faida ya wakazi wa hapa Kisauni.” Alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi huo Mohammed Islam amesema mradi huo utawanufaisha zaidi vijana wa eneo hilo na maeneo mengine ya kaunti huku akiwahimiza vijana kusomea taaluma ya kiufundi ili kunufaika pakubwa na miradi sawia.

Mradi huu utachukua vijana wafanyakazi kutoka hapa hapa na hakuna wa kutoka nje. Tuzinatie elimu ni muhimu sana kusomea taaluma za ufundi ili kunufaika, lakini pia kazi zile nyingine kama mradi huu tungependelea kuelimisha vijana wetu wa hapa kwetu,” alisema.

Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba amesifia mradi huo akisema hatua hiyo itafungua njia kwa wawekezaji wengine kuwekeza katika eneo hilo na kupeana ajira kwa vijana.

Sifa ya zamani Kisauni ilikuwa sifa kila mtu akiikwepa, lakini sifa ya sasa ni tofauti na ishara kwamba kuna amani na tuna imani wawekezaji wengine watakuja eneo hili ili kusudi vijana wetu wapate ajira.

Nawashukuru sana na niwaombe m wachukue vijana hawa kuanzia kuchimba msingi hata kuinua majengo hadi majumba kukamilika ili vijana wetu wapate ajira.” Alisema.

Naye Aboud Jamal Mwenyekiti wa shirika la kitaifa la kibiashara KNCCI tawi la Mombasa ameupigia upato mradi huo akiutajia kuwa wa nafuu na kuchangia kuboresha ukuaji wa uchumi.

Mradi huo wa nyumba za makazi ya kisasa kwa bei nafuu unatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya uzinduzi kufanyika, huku nyumba zaidi ya 816 zikitarajiwa kujengwa, sura na mandhari ya Kisauni yakitarajiwa kubadilika.

Utakuwa mradi wa kwanza na wa kipekee wa nyumba za kisasaa katika eeo hilo.

BY MJOMBA RASHID