Watu 25 wakiwemo wanajeshi 14 wameuawa katika mlipuko kwenye kituo cha treni katika wilaya Balochistan nchini Pakistan, huku mamia ya wengine wakiripotiwa kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi Mlipuko umetokea wakati abiria wakisubiria usafiri wao katika mji wa mkuu wa wilaya ya Balochistan, eneo jirani na mataifa ya Afghanistan na Iran.
Afisa Mkuu wa Polisi katika eneo hilo Mohammed Baloch amethibitisha hayo akisema idadi hiyo imeongezeka kutoka watu 22 walioripotiwa kufariki mapema Jumamosi.
Mamlaka imeliambia shirika la habari la AFP kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka wakati huu waliojeruhiwa wakiendelea kupokea matibabu.
Wilaya ya Balochistan na yenye idadi kubwa ya watu nchini Pakistan na inakaliwa na makundi ya watu wanaotaka kujitenga, wilaya hiyo pia ikiwa na utajiri wa rasilimali.
Kikundi cha watu kinachopigania kujitenga kwa eneo hilo kimedai kuhusika na mlipuko huo huku maaafisa wa polisi wa kituo cha Quetta wakisema wameanzisha uchunguzi kubaini kiini cha mlipuko huo ambao wanasema huenda ikawa umtokana na mlipuaji wa kujitoa mhanga.
Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif amelaani shambulio hilo akisema magaidi waliohusika kuwaua na kuwajeruhi raia watakabiliwa vilivyo.
BY AFP