HabariLifestyleWorld

Afueni ya Likizo; Skyward Express Yatangaza kiwango cha chini cha Nauli kwa safari za Ndege kuelekea Dar es salaam

Ni afueni kwa abiria wanaolenga kutumia usafiri wa anga kutoka Uwanja wa Ndege wa Moi jijini Mombasa kuelekea Dar es Saalaam, Tanzania kufuatia punguzo la nauli kwa kiwango cha chini.

Hii ni baada ya kampuni ya Skyward Express kutangaza kiwango cha chini kabisa cha nauli kitakachoanza kutumika kwa abiria wanaotumia kampuni hiyo kuanzia Disemba 11, 2024.

Katika taarifa yake Skyward imesema kwamba abiria hao watakuwa wakilipa nauli ya kuanzia shilingi 16,610.

Safari hizo ambazo ni za kupitia ndege inayotoka Uwanja wa JKIA jijini Nairobi zitakuwa kila Jumatano na Jumamosi kila wiki.

Haya yanajiri huku Kampuni ya Skyward Express ikiendeleza safari za moja kwa moja kutoka Uwanja wa JKIA, Nairobi hadi Dar es Salaam, Tanzania kila Ijumaa, Jumapili na Jumatatu kila wiki abiria wakilipa nauli ya kiwango cha chini kabisa ambacho ni kuanzia shilingi 18,500.

By Mjomba Rashid