HabariMombasaNews

Usalama Kuimarishwa zaidi kaunti ya Kilifi msimu huu wa likizo na sherehe za Kufunga Mwaka

Hali ya usalama imeimarishwa kaunti ya Kilifi maandalizi ya msimu huu wa sherehe za Krisimasi na kufunga mwaka yakiendelea maeneo tofauti tofauti kaunti hiyo.

Maandalizi ya msimu wa sherehe za Krisimasi na mwaka mpya yanaendelea kwa njia tofauti tofauti kaunti ya Kilifi, huku mikakati ya kudumisha usalama ikiwekwa imara kaunti hiyo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Joseph Ongaya, mikakati ya kiusalama iliyowekwa inalenga kuondoa hofu yoyote ya kiusalama hasa katika maeneo ambayo yamekuwa yakishuhudia visa vya uhalifu.

Amesema wakati mikakati hiyo inapoendelea kutekelezwa wakazi kaunti ya Kilifi wanafaa kushirikiana na maafisa wa polisi kupiga ripoti iwapo kuna mambo yaliyokinyume cha sheria yanafanyika, ili kuhakikisha usalama unazidi kudumishwa.

Nawahakikishia ya kwamba kaunti ya Kilifi tuko tayari tumeweka mikakati tunaielewa vyema kaunti yetu tunajuwa palipo na taashishwi za kiusalama na hapo awali ambapo kumekuwa na shida lakini leo hii katika ratiba ya kazi ya kila siku tunaketi pamoja na kujadiliana kuona mpangilio wetu umefanikiwa kwa kiwango gani na unaendelea kufanya kazi kwa kiwango gani.” alisema Ongaya

Aidha ametoa hakikisho kwa wakazi wa Kilifi na wageni wanaopanga kuzuru kaunti ya Kilifi kuondoa shaka la utovu wa usalama kwani kila kitu kiko shwari akiongeza kuwa maafisa wa polisi wako tayari kukabiliana na tukio lolote la utovu wa usalama.

Nawahakikishia ni nimewaelezea mninukuu tuko tayari njooni hali ya usalama iko sawa njooni mjivinjari kwani huu ndio muda wa kufanya hivyo ufurahie bila wasi wasi.” alisema Ongaya.

Erickson Kadzeha.