HabariNews

Jeshi La Wanamaji La Kenya Navy Na La Pakistan Watoa Huduma Za Matibabu Ya Bure Mvita

Wanajeshi wa jeshi la wanamaji kutoka Pakistan na wale wa hapa nchini leo wamejitosa eneo la mvita, katika Kliniki ya Mvita kaunti ya Mombasa kutoa huduma za matibabu ya bure kwa wakazi wa Mvita na Mombasa kwa jumla.

Hii ni baada ya meli ya kijeshi iliyosheheni vifaa vya matibabu na dawa kutua Mombasa tayari kutoa huduma mbali mbali za matibabu pamoja na wataalamu wa kijeshi, matabibu wa jeshi la wanamaji la Kenya ya ni Kenya Navy na Pakistan Navy.

“Tungependa kutoa huduma hizi kwa watu wa Mombasa maana tuawapenda sana” amesema nahodha wa meli ya PNS MOAWIN Humayun Yaqoob.

Humayun Yaqoob, Nahodha wa meli ya PNS MOAWIN

Mamia ya wakazi wa Mombasa wakiwemo kina mama, watoto na wazee wamejitokeza kufanyiwa ukaguzi na matibabu ikiwemo vipimo vya macho, masikio, koo, kisukari, afya ya uzazi, na vipimo vya kimaabara kwa usimamizi wa kaunti ya Mombasa.

“Ujio wa meli hii Mombasa si mara ya kwanza, hii ni mara ya tatu hapa Mombasa na tunashukuru kwa usaidizi huu wa Pakistani, kwani imeonyesha wanavyojali wakazi wa Mombasa kwa kuwapunguzia gharama za matibabu ambayo yapo ghali mno.” Afisa mkuu katika wizara ya afya Khadija Shikely amesema.

Khadija Shikely, Afisa Mkuu katika wizara ya afya Kaunti ya Mombasa

Ni shughuli inayotarajiwa kufanyika kwa siku mbili huku kanali Inam akihakikisha kuwa kila mmoja atahudumiwa vizuri kabla zoezi hilo kukamilika.

Aidha kanali JJC Wambugu kutoka jeshi la wanamaji hapa nchini, lenye makao yake mtongwe, likoni kaunti ya Mombasa ameeleza kuwa zoezi hili linakuja kama mikakati ya matayarisho ya maadhimisho ya siku ya jeshi la wanamaji ambayo hufanyi kila tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.

Kanali JJC Wambugu, Kenya Navy

Wambugu ameeleza kuwa hii ni njia moja yakuendeleza uhusiano mwema kwa jamii ya Mombasa ambako jeshi la wanamaji wana makao yake makuu huku akileeza kuwa wamefanya haya pia kaunti ya Kwale na Lamu.

BY SOPHIA ABDHI