HabariNews

Wakazi Wa Mombasa Kufaidika Na Huduma Za Matibabu Za Bure Baada Ya Meli Ya Kijeshi Ya Matibabu Kutua Mombasa

Mgeni njoo mwenyeji apone ni msemo uliopata maana baada ya meli ya kijeshi ya PNS MOAWIN kutua katika bandari ya Mombasa muda wa saa tatu asubuhi siku ya Jumatano.

Meli hiyo ilipokelewa na wenyeji wake raia wa Pakistan wanaoishi humu nchini, maafisa wa polisi wa hapa nchini na wanajeshi wenza kutoka hapa nchini wa jeshi la wanamaji imeonekana kutua na matumaini yamatibabu.

“Tumekuja kusaidia ndugu zetu hapa kenya kupata matibabu mbalimbali . Hii ni ziara yetu ya tatu hapa nchini kenya na tunataamiakuhudumia wananchi kwa vifaa vya matibabu pamoja na dawa za matibabu tulizobeba katika meli hii” asema nahodha wa meli hiyo Humayun Yaqoob.

Captain Yaqoob ameeleza kuwa kuna zaidi ya wataalam 9 wa maradhi tofauti pamoja na vifaa na dawa ambazo wamekuja nazo kushirikiana na wataalam wa jeshi la wanamaji hapa nchini kuwafanyia ukaguzi ikiwemo ule wa kimaabara kwa wale watakaohitaji huduma mbalimbali.

Aidha Kanali Iman amewarai wakazi wa Mombasa kujitokeza kwa wingi ili kupata matibabu hayo sawia na kufaidika na ujio wa meli hiyo ya kimatibabu.

Kwa upande mwengine ziara ya wanajeshi hao imeonekana kupiga jeki uchumi wa kaunti ya Mombasa maana muda mfupi baada a kutua, wameonekana kuingia mjini wakiuliza sehemu mbali mbali za kuzuru kuitalii ili wafahamu vyema mji wa Mombasa na kupata kumbukumbu wanapo rudi Pakistan.

BY SOPHIA ABDHI