HabariNews

Mshukiwa Sugu wa Ulanguzi wa Dawa za Kulevya Anaswa Kisauni

Mshukiwa sugu wa ulanguzi wa mihadarati amekamatwa eneo la Utange eneobunge la Kisauni kaunti ya Mombasa.

Anita Michael amenaswa nyumbani kwake na maafisa wa kupambana na dawa za kulevya akiwa na dawa nyingine za kulevya.

Anita amenaswa na makachero kufuatia kudokezwa taarifa zake na wananchi eneo hilo.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wenyeji walikuwa na wasiwasi na kuingiwa na shauku kutokana na msongamano wa vijana waliokuwa wakitembelea nyumbani kwake.

Wakimtembelea mshukiwa kabla ya mapambazuko, maafisa hao walinasa vidonge 100 vya unga wa hudhurungi na kiasi cha bangi inayoshukiwa. Pia zilizonaswa ni pesa zinazoaminika kuwa mapato ya biashara yake,” DCI ilisema katika taarifa.

Katika taarifa yeke Idara ya upelelezi DCI imewapongeza wakazi kwa kuwadokeze taarifa kuhusu mshukiwa huyo huku ikihimiza zaidi ushirikiano.

Mshukiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Bamburi akisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu juma lijalo.

Maafisa wa polisi wanaendeleza uchunguzi zaidi.

By Mjomba Rashid