HabariNews

Rais Ruto Awaonya Wanakandarasi Wazembe wanaochelewesha Miradi muhimu ya Serikali.

Rais William Ruto ametoa onyo kali kwa wanakandarasi wanaochelewesha utekelezaji wa miradi muhimu ya serikali.

Akizungumza huko kaunti ya Kisii wakati wa ukaguzi wa wa ujenzi wa kituo cha saratani cha Kisii, Rais amesema serikali imejipanga kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, akisema wakandarasi wanaohujumu juhudi zake hawatavumiliwa.

Kuna wakandarasi wengi wanatuangusha, na hatutawaruhusu. Huu ni mwaka wa kuwasilisha ajenda zetu kama tulivyopanga,” alisema.

Alieleza kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Rais Ruto alimwagiza mwanakandarasi huyo kutekeleza mradi huo kuambatana na makubaliano la sivyo akabiliane na kusitishwa kwa kandarasi hiyo.

Umelipwa pesa zote zinazohitajika. Hakuna sababu yoyote kwa nini mradi huu hauendelei,” alisema.

By Mjomba Rashid