AfyaHabariNews

Idadi ya Maambukizi ya Virusi vya Mpox Yaongezeka; Wizara ya Afya Yapania Kutoa Chanjo

PHOTO COURTESY

Wizara ya afya imetangaza kuwa inapania kuanza kutoa chanjo ya virusi vya ugonjwa wa ndui ya nyani (Mpox).

Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa waathiriwa ambao wengi wao ni madereva wa masafa marefu.

Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amebaini ongezeko la idadi ya wagonjwa wa virusi hivyo vya Mpox ambapo kufikia sasa Kenya imethibitisha visa 36, baada ya kesi nyingine 5 mpya kubainika.

Akizungumza na wanahabari, Katibu huyo wa afya ya umma katika Wizara ya afya amesema kuwa kaunti ya Nakuru inaongoza kwa visa 10, Mombasa 8 na Busia visa 3, huku Taita Taveta Kilifi na Kericho zikinakili kesi moja mpya ya ugonjwa huo.

Aidha Muthoni ameeleza kwamba Wizara ya afya imeWeka mikakati mbalimbali kukubiliana  na ugonjwa huo kutoenea sehemu mbalimbali nchini hasa mipakani.

By Mjomba Rashid