Mahakama Kuu imekataa ombi la Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi wa DCI kutupilia mbali agizo la kuwataka wafike kortini kueleza waliko Wakenya watatu waliotekwa nyara.
Hii ni kufuatia ombi la wakili wa Wakuu hao Paul Nyamondi kutaka kutupiliwa mbali kwa maagizo hayo kwa madai kuwa ombi na maagizo hayakuwa yametolewa vyema kwa wateja wake.
Katika uamuzi wake Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita amesema kuwa Inspekta Mkuu Douglas Kanja na Mkuu wa DCI Mohammed Amin walipokea maombi hayo ipasavyo na agizo lililotolewa Januari 8 kupitia barua pepe zao.
Aidha Hakimu amegundua na kusema kwamba wote wawili pia wangeweza kumuagiza wakili wao kuwawasilisha.
Hakimu huyo pia amekataa ombi la wakili Paul Nyamondi la kusimamisha utekelezaji wa uamuzi huo unaosubiri rufaa huku akimpa siku 14 Inspekta Jenerali kuwatoa Mateka wa Mlolongo.
Hata hivyo Jaji Chacha amewaagiza wawili hao wajiwasilishe mahakamani Januari 30 wakati wa kusikilizwa kwa ombi ambalo limewasilishwa na LSK kwa madai ya kesi za utekaji nyara.
By News Desk