KimataifaNews

Ukraine Yashirikiana na Uingereza na Lithuania Kuzindua Mfumo wa Kufuatilia Nafaka Zilizoibiwa

Ukraine imetia saini mkataba na mataifa ya Uingereza na Lithuania katika kutekeleza Mpango wa Kuthibitisha Nafaka, (GVS).

Katika Mkutano wa Mawaziri wa Kilimo wa Berlin, Waziri wa Sera ya Kilimo na Chakula wa Ukraine Vitalii Koval ametia saini Mkataba huo na mawaziri wenziwe wa kufanikisha mpango huo unaolenga kushughulikia na kuzuia usafirishaji haramu wa nafaka za Kiukreni kutoka kwa maeneo yaliyochukuliwa.

Haya ni kwa mujibu wa Chombo cha habari cha Wizara ya Sera ya Kilimo na Chakula ya Ukraine, kama ilivyoripotiwa na Ukrinform.

Waziri Koval ameutaja Mkataba huo kama hatua ya kwanza katika ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu kati ya Ukraine na Uingereza, ambao utakuwa msingi wa ushirikiano katika karne ijayo.

Utekelezaji wa majaribio ya mpango huu utafanyika nchini Lithuania – katika bandari ya Klaipeda, ambayo itakuwa kitovu muhimu cha kuthibitisha asili ya bidhaa za kilimo za Kiukreni,” Vitalii Koval alisema.

Kulingana na waziri wa Ukraine, Mpango huo wa GVS utaruhusu kutambua nafaka zilizoibiwa na kusitisha usafirishaji haramu wa nafaka hizo.

Mkataba huo pia unatoa hifadhidata ya ubunifu kutoka Uingereza: teknolojia za hali ya juu za kuamua mahali pa kulima zitasaidia pia kulinda maslahi ya wakulima wa Ukreni na uwazi wa soko.

Wakati uo huo Waziri Koval alitoa shukrani kwa washirika wa kimataifa kwa imani na msaada wao, akisisitiza kwamba ushirikiano huu kati ya Ukraine, Uingereza, na Lithuania unaimarisha uwazi katika soko la kilimo na kulinda maslahi ya wakulima wa Ukraine.

Kama ilivyoripotiwa na Ukrinform, Ukraine na Uingereza aidha zilitia saini makubaliano ya kihistoria ya miaka 100 ili kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi.

By Ukrinform