Rais William Ruto amekariri kuwa mipango imekamilika tayari kununua ardhi zenye utata ili kabiliana na tatizo sugu la uskwota maeneo mbalimbali ya ukanda wa Pwani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chuo cha akiufundi cha Likoni rais amesema serikali ishaweka tayari fedha za kununua ardhi zenye utata katika eneo hilo.
Kiongozi huyo wa taifa amebaini kuwa kilichosalia sasa ni kwa viongozi wa pwani kuwasilisha orodha ya maeneo yanayokabiliwa na tatizo hilo la uskwota ili serikali isuluhishe na kurudishsa ardhi hio mikononi mwa wenyeji.
“Hapa Pwani bado uskwota unatusumbua sana na hii serikali itatatua tatizo sugu ya manbo ya uskwota na ardhi pwani ya Kenya, na nimeshakubaliana na viongozi wote wa pwani wakinipatia priority list tayari pesa ya kulipia ile absentee landlords na tuwapatie mashamba yenu iko tayari, kwa hivyo tutashughulikia tatizo la ardhi hapa…” akasema.
Kadhalika rais ametoa onyo kali kwa madalali na mabwanyenye wanaonyemelea ardhi za umma ikiwemo ardhi ya chuo cha kiufundoi cha Likoni akiwataka wakome vingenevyo watakabiliwa kisheria.
By Mjomba Rashid