HabariNews

NLC yakita kambi Mombasa ili kuskiliza vilio vya walalamishi wa maswala ya ardhi

Tume ya ardhi NLC kwa mara nyengine tena imekita kambi katika kaunti ya Mombasa ili kuskiliza vilio vya walalamishi wa maswala ya ardhi.
Tume hiyo ambayo inaongozwa na kaimu mwenyekiti ambaye pia ni kamaishna wa tume hiyo professor James K. Tuitoek imeeleza kuwa kuna haja ya kufanya zoezi hilo tena kwani awali baadhi ya walalamishi na washtakiwa hawakuweza kufika katika vikao vya awali .
Hatahivyo mvutano baina ya wamiliki wa ardhi na wakaazi wa baadhi ya maeneo ya mombasa unatarajiwa kupata suluhu kupitia vikao hivi kama wanavyoeleza baadhi ya walalamishi walioweza kufika katika vikao hivyo.
Kwa upande mwengine aliyekuwa meya wa kaunti ya Mombasa Rajab Sumba ambaye pia alifika katika kikao hicho kuwakilisha baraza la wazee wa Mombasa ameeleza kuwa inasikitisha kuona wakazi wa Mombasa wanavyohangaishwa na mabwenyenye huku akilaumu baadhi ya viongozi waliomamlakani kukosa kutatua kesi hizi .
Kwa upande wake afisa wa maswala ya dharura katika shirika la Haki Africa Mathias Shipeta ameeleza matumaini ya kupata haki kwa wakazi wa pwani kupitia tume hiyo akitaja kuwa kupitia
tume hiyo wataweza kuwasilisha ushahidi wa kutosha walionao kutetea haki ya umiliki.
Tume hiyo ya NLC itakuwa Mombasa kwa siku mbili kusikiza malalamishi ya dhulma za ardhi kwa siku mbili wakiahidi kuwa pande zote husika zitapata fursa ya kusikizwa kabla uamuzi kutolewa.

By Sophia Abdhi