LifestyleMombasaNews

Zaidi ya Familia 2,000 Pwani Kunufaika na Msaada wa Ftari kutoka kwa Bamburi Cement

aidi ya familia 2,000 zisizojiweza eneo la Pwani zimeratibiwa kunufaika na msaada wa chakula katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Familia hizo kutoka kaunti za Mombasa, Kwale na Kilifi, zitapokea ugavi wa chakula kutoka kwa kampuni ya Saruji ya Bamburi Cement chini ya usimamizi mpya wa kampuni ya Amsons Group.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa shughuli ya ugavi huo wa chakula katika kaunti ya Mombasa  Mkurugenzi wa Mauzo katika Kampuni ya Bamburi Cement Martin Kariuki amesema kuna Waumini wengi nchini Kenya ambao wanapitia changamoto za kimaisha hivyo basi kuwepo haja ya kuwasaidia hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Tunataka kusaidia zaidi ya familia 2,000 ukanda huu wa pwani baada ya kuangalia na kuona kuna watu wengi wanaoteseka hasa wakati huu ambapo hali ya uchumi sio nzuri.”

Tumenza na 2,000 na tunatarajia kuongeza idadi hiyo zaidi na tunaomba wahisani wengine wajitokeze kuwasaidia wasiojiweza sio tu katika mwezi huu wa Ramdahan bali hata nyakati zengine ili wote wanaoathirika na njaa wapate afueni.” Kariuki alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Amsons Group Tawakal Rajab Sumba amesema wataendelea na harakati hizo na ushirikiano mwafaka ili kusaidia na kuwaenua wakenya kimaisha katika maeneo mbalimbali huku wakilenga shule, vituo vya watoto yatima na jela.

“Tunachukua ahadi ya kushirikiana na wahisani zaidi kwa nia ya kusaidia kuboresha maisha ya wale wasiojiweza hivyo basi,tunawaomba wananchi mtupokee na mtuunge mkono ili tufuzu katika hii safari mpya tulioanza na tuweze kufikia makundi zaidi ya watu.” Alisema Sumba.

Naye Zubeir Noor ameishkuru kampuni ya Bamburi cement kwa kuwasaidia wakenya kwa njia iliyo na taratibu nzuri huku akizitaka kampuni mbalimbali kuiga harakati hizo za kuwasaidia wasiojiweza .

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwaleta Bamburi cement kwa mara ya kwanza kugawa riziki kwa njia ya kistaarabu wakati kama huu ambapo hali ya uchumi ni ngumu na tunatumai hatua hii itataoa changamoto kwa taasisi na mashirika mengine kutoa msaada wa aina hii hapo mbeleni.” Alisema Noor.

Mpango huo wa Ugavi wa chakula cha ftari ni mara ya kwanza kutekelezwa na kampuni ya Bamburi cement iliyo kwa sasa chini ya Amsons Group kutoka Tanzania.

Katika mpango huo, Familia kati ya 4,000 hadi 5,000 katika kaunti tatu eneo le Pwani, na kaunti ya Nairobi na Machakos zimeratibiwa kufaidika na ufadhili huo wa chakula.

BY MJOMBA RASHID