Mradi wa ujenzi na ukarabati wa reli ya zamani kuunganisha usafiri wa abiria kutoka katikati ya mji wa Mombasa hadi kituo cha reli ya kisasa cha SGR Miritini utaendelea.
Haya ni kwa mujibu wa Katibu katika idara ya uchukuzi Mohammed Daghar, licha ya mradi huo kukumbwa na pingamizi kutoka kwa serikali ya kaunti ya Mombasa hasa kuhusu fidia ya wakazi watakaoathirika.
Akizungumza mjini Mombasa mnamo Jumatano Daghar alisema mradi huo ulinuwia kuchukua mwaka mmoja ulikubwa na changamoto ya ukosefu wa ardhi huku akibaini kuwa tatizo hilo limetatuliwa.
“Tulikuwa na changamoto ya ardhi na usahihi wan jia ya mradi huu, kwani kilomita 1.4 ilikuwa ni hadi ipatikane, hivyo kutokana na hilo Wizara yangu imetoa fedha zilizotakiwa na mradi ulikuwa umesima katika asilimia 65 hivyo hatuko mbali kukamilisha,” alisema.
Daghar alisema mradi huo utakaogharimu takribani shilingi bilioni 4.2 utarahisha shughuli za usafiri na kutengeneza nafasi za kazi kwa vijana na kina mama wafanyibiashara.
“Manufaa ya mradi huu utatoa fursa kwa abiria wa vituo vyote saba vya SGR wanaondoka kutoka Mombasa kuwarahisishia usafiri wao kutoka katikati ya jiji hili kwa urahisi,” alisema Daghar.
Wakati huo huo Daghar alibaini kuwa serikali haitaruhusu mtu yeyote kuhangaisha watekelezaji wa miradi ya serikali akiongeza kuwa tayari idara yake imefanya mazungumzo na idara ya usalama kuhakisha usalama unaimarishwa wakati wa mradi huo.
BY EDITORIAL