HabariKimataifaNews

Tanzania yasheherekea miaka 60 ya uhuru.

Rais Samia analiongoza taifa lake katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye atayekuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo inayofanyika katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam.
Wageni wakuu wanaohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Filipe Nyusi wa Msumbiji, Mwenyekiti wa AU , Rais wa DRC Felix Tshisekedi na Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda. Wengine ni wawakilishi waliotumwa na mataifa yao .
Mkesha wa kuamkia sherehe hiyo ya kitaifa , Rais Samia alihutubia taifa ambapo alitaja mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu Tanzania ilipopata uhuru na kueleza matumaini yake kwa zaidi, miaka ijayo.
Akilinganisha mahali nchi ilipo kwa sasa, alisema Tanzania ina mafanikio katika miundombinu, kwa mifano ya maendeleo katika usafiri wa anga na reli, na kuhainisha mabadiliko makubwa katika huduma za kijamii kama elimu na afya.

BY NEWSDESK