Waziri wa elimu kaunti ya Kwale Ndegwa Mangale Chiphoromodo, amewahakikishia wanafunzi wote waliofanya mitihani ya KSCE 2020 na kufaulu kwamba watajiunga na vyuo vikuu nchini bila malipo.
Akizungumza na meza yetu ya habari kupitia njia ya simu kwenye kipindi cha sauti asubuhi Ndegwa amesema kwamba serikali ya kaunti kupitia idara ya elimu imetenga fedha za kutosha kufanikisha ajenda hiyo.
Aidha ametoa pongezi kwa wanafunzi pamoja na washikadau katika kaunti hiyo kwa matokea bora ambayo kulingana na yeye haijawahi kutoa katika kaunti hiyo.
Wakati huo huo kiongozi huwa amewaomba viongozi hasa kutoka ukanda wa Pwani kuja pamoja ili kuboresha sekta ya elimu kama inavyoshuhudiwa kaunti ya kwale badala ya kutoa lalama zisizo na msingi.
Kaunti ya kwale ni miongozi mwa kaunti nchini hasa kutoka ukanda wa Pwani zilizofanya vyema katika mitihani ya kitaifa ikizingatiwa kwamba kwale pekeake imetoa zaidi ya wanafunzi 400 watakao kwenda katika vyuo vikuu.
By Reporter David Otieno