HabariSiasa

Rais wa LSK asisitiza kwamba katiba ya Kenya haipaswi kurekebishwa….

Huku rufaa ya kupinga uamuzi wa mahakama ya juu ikitarajiwa kuwasilishwa rasmi mahakamani wiki hii, rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Nelson Havi amesema katiba ya Kenya haina dosari yoyote hivyo hakuna haja ya kufanyiwa marekebisho.

Akijohiwa na kituo kimoja cha radio humu nchini, Havi amesema utawala wa sasa unapaswa kuzingatia pakubwa utekelezwaji kikamilifu wa katiba na wala sio kuifanyia marekebisho.

Kuhusu uamuzi wa wiki iliyopita wa majaji watano wa mahakama ya juu kuhusu kuharamishwa kwa BBI, Havi amesema anaunga mkono uamuzi huo kwani unaendana na katiba.

By Warda Ahmed