Visa vya dhulma za kijinisia vimeongezeka kwa kiwango kikubwa kaunti ya Kwale tangu kuchipuka kwa janga la corona nchini.
Afisa wa wizara ya masuala ya kijinisia nchini kaunti hiyo Nelly Amoite amesema kuwa visa vya mizozo ya kinyumbani na mimba za mapema vimekithiri.
Akizungumza katika eneo la Diani, Amoite amesema kwamba kesi nyingi haziripotiwi kutokana na masuala ya dini na mila potofu.
Afisa huyo amebainisha kuwa serikali inaendelea kuihamasisha jamii ili kukomesha visa hivyo ambavyo vimewaathiri pakubwa wanawake.
Amewataka akina mama kuchukua fedha za serikali walizotengewa ili wazifanyie biashara huku watoto wa kike wakitakiwa kwenda shule ili kuepuka visa vya mimba.
By Kwale Correspondent