Wanafunzi wote waliofanya mtihani wa darasa la nane KCPE watapata nafasi za kujiunga na shule za sekondari kuanzia tarehe mbili ya mwezi agosti mwaka huu.
Akitangaza matokeo ya uteuzi wa shule ambazo wanafunzi hao wameteuliwa kujiunga, waziri wa elimu Prof George Magoha amesisitiza kwamba hakutakuwa na uteuzi wa wanafunzi katika ngazi ya kaunti kama ilivyokuwa hapo awali.
Waziri Magoha aidha ametangaza kwamba idadi ya watoto wa kike wanaojiunga na shule za upili mwaka huu iko juu zaidi kuliko wa kiume.
Amesema kuwa watoto wote wa kike ni lazma wajiunge na shule za sekondari, wawe wajawazito ama wamejifungua.
Hata hivyo ili mwanafunzi kujua shule aliyoteuliwa, mwanafunzi anatakiwa kutuma nambari ya usajili kwa:22263
Wakti huohuo Magoha amesitisha utumizi wa mabasi ya shule katika shughuli za kibinafsi akisema ni njia mojawapo ya kuwalinda wanafunzi dhidi ya virusi vya Corona.
Magoha amewataka wote wanaotaka kutumia mabasi hayo kupata idhini kutoka kwa wizara ya Elimu.
By Joyce Mwendwa