Huenda msajili wa vyama vya kisiasa akawa na mamlaka ya kukataa vyama vilivyo na majina au nembo ambazo zinakiuka maadili, iwapo mswaada wa marekebisho ya sheria utapitishwa na seneti.
Bunge la kitaifa lilikataa pendekezo lililowasilishwa na mbunge wa kandara Alice Wahome, akitaka kifungu hicho cha saba kiondolewe akidai kwamba kinakiuka uhuru wa vyama vya kisiasa.
Wabunge 142 walipiga kura kupinga pendekezo hilo huku 15 pekee wakiunga mkono, baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono naibu wa rais waliondoka kikaoni hata wakati ambapo kura hizo zilikuwa zikipigwa.
Ikumbukwe kwamba bunge limehairisha vikao hadi January 25 ambapo litaendelea na mjadala kuhusu mswada huo ambao, umezua hisia baina ya wabunge wa kieleweke na tangatanga.
BY NEWSDESK