AfyaHabariLifestyleMombasaNews

Mashirika ya kutetea haki za watoto yabuni miradi ya kimasomo Eneo la Pwani.

Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za watoto katika eneo la Pwani yamebuni miradi ya kimasomo itakayowaepusha watoto na biashara ya ngono.
Kulingana na meneja wa mradi wa building a future project kutoka shirika la Teredes homes Netherlands Godfrey Kibet watoto hao wanaweza kusalia shuleni kupitia karo na sare za shule.
Kibet aidha amesema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuwarudisha watoto waliaothirika na biashara hiyo ili kuendeleza masomo yao.
Kando na hayo afisa mkuu wa masuala ya kijamii ya shirika la Kesho Kenya Ruth Mugira amesema shirika hilo limeanzisha miradi mbalimbali ya kuhakikisha masomo watoto hayaathiriki na biashara ya ngono.
Wakati huo huo amebainisha kuwa miradi hiyo pia inalenga kuwaelimisha watoto ili waweze kujitegemea kimaisha.