HabariNews

raila Odinga sasa anaitaka Marekani kuharakisha na fidia kwa wahasiriwa wa shambulio la kigaidi lililotekelezwa hapa nchini mwaka 1998.

Mpeperusha bendera wa chama cha muungano wa Azimio one Kenya raila Odinga sasa anaitaka serikali ya Marekani kuharakisha na kuwafidia wahasiriwa wa shambulio la kigaidi lililotekelezwa hapa nchini mwaka 1998.
Kauli ya Raila inajiri siku chache baada ya mkutano na wawakilishi wa waathiriwa hao jijini Washington DC wakati wa ziara yake nchini Marekani.
Msemaji wa kamati ya kiufundi wa kampeni za Raila-Prof Makau Mutua, anasema wawakilishi hao walihongwa na mwanasheria mkuu wa Marekani Phillip M. Musodino.
Prof. Mutua anasema raila analenga kushinikiza Sheria kufanyiwa marekebisho ili kujumuisha waathiriwa wa Kenya na familia zao miongoni wa wanaofaa kufidiwa.
Baada ya miaka 20 baada ya shambulio hilo lililotekelezwa katika ubalozi wa marekani hapa Nchini, waathiriwa wamekuwa wakilalamikia hatua ya Marekani kujikokota katika kuwafidia.

BY EDITORIAL DESK