Mwanaharakati na mtetezi wa haki za kibinadamu katika Muungano wa OKOA MOMBASA, Mesh Abdul amepinga vikali hatua ya maafisa wa kaunti katika kaunti ya Mombasa kuwahangaisha wafanyanyabiashara wadogowadogo.
Akizungumza na wafanyabiashara hao eneo la Mwembe tayari, Abdul ambaye ni mgombea huru wa kiti cha Mwakilishi wadi katika wadi ya majengo kaunti ya Mombasa, amesema kwamba mahangaiko ya wafanyakazi hao pamoja na wale wa jua kali yanatokana na viongozi wsiojali mahitaji ya wananchi wa chini kutelekeza majukumu yao, licha ya kuchangia pakubwa uchumi wa taifa.
Wakati uo huo Abdul amewataka wananchi kuwachagua viongozi wanaoelewa changamoto zao, huku akiwarai wakaazi wa wadi ya Majengo Mwembe Tayari kumpigia kura katika uchaguzi wa agosti 9 ili kuwapigania haki zao za msingi.
>> news desk