HabariNews

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameondoa wasiwasi kwa umma uliodhani angetangaza hatua za karantini.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameondoa wasiwasi kwa umma uliodhani angetangaza hatua za karantini katika hatua za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola.

Rais Museveni amelezea kuwa hapana haja ya kuweka vizuizi kwa sababu ameona pana urahisi kudhibiti maambukizi ya Ebola ikilinganishwa na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Kiongozi huyo wa Uganda amesema kwenye hotuba yake kwamba kulingana na takwimu za wizara ya afya ni watu watano ndiyo wamethibitishwa kufariki kutokana na mlipuko wa Ebola tangu wizara hiyo ilipotangaza rasmi kwamba ugonjwa huo umegunduliwa nchini Uganda.

Waathirika kwa jumla ni 31 na kwamba kwa sasa idadi kubwa ya waathirika wamo katika wilaya tatu zilizo jirani.

BY EDITORIAL TEAM.