Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea wasi wasi wao kufuatia ongezeko la visa vya ulanguzi wa binadamu katika eneo la Pwani.
Kulingana na takwimu za shirika la kijamii la Trace Kenya, takriban visa elfu 12 vya ulanguzi huripotiwa kila mwaka katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa shirika hilo Paul Adhoch amesema kwamba kaunti ya Kwale inaongoza na takriban visa elfu 4 vya ulanguzi wa watoto.
Kwa upande wake afisa wa shirika la Peace Tree Network (PTN) Rachel Akinyi amesema kuwa visa hivyo vimekithiri katika maeneo ya kitalii kaunti hiyo.
Akinyi amedokeza kwamba waaathiriwa wa visa hivyo hutumika katika biashara ya ngono ili kukidhi mahitaji ya familia yao.
BY EDITORIAL TEAM