HabariNews

Mashirika Yashinikiza Serikali Kukarabati Majengo Marefu Kuwarahisishia Walemavu Kuyafikia

Mashirika yasiyo ya kiserikali eneo la Pwani yamewasilisha Mswada wa Mapendekezo yanaotaka majengo kukarabatiwa ili kuwezesha jamii zinazoishi na ulemavu kufikia huduma za msingi katika afisi za serikali na kibinafsi.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Zedekiah Adika mashirika hayo yameeleza kughadhabishwa kwao na jinsi afisi nyingi zinazopatikana katika majumba ya ghorofa ambayo yanakosa njia zinazoweza kutumiwa na watu wenye ulemavu licha ya viongozi kufahamu hayo.

“Tulianza mchakato huu miaka 3 nyuma na hata kuwaandikia barua afisi husika kulalamikia ugumu wa kufikiwa ofisi hizi na jamii ya walemavu. Na majumba mengi ni ya Kiserikali lakini bado hawajashughulikia kuwarahisishia,” akasema Bw. Adika.

Adika ameongeza kuwa mswada huo kadhalika unalenga kugatua baadhi ya majengo kaunti hiyo ili kurahisisha ukarabati wa majengo hayo.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Zamzam Mohammed aidha ameeleza masikitiko yake kutokana na dhulma wanazozipitia watu walio na ulemavu akihakikishia mashirika hayo kwamaba mswada huo utafaulu bungeni.

“Walemavu wamekuwa wakiangaliwa kwa jicho la dharau katika serikali hii, hata ukiangalia katika kampuni na mshirika walemavu wanafaa kupewa kipaumbele lakini sasa ukiangalia katika walemavu huwezi kupata walemavu.”Amesema Zamzam.

Zamzam amesema atapeleka suala hilo bungeni ili kuhakikisha walemavu wanapata haki yao.

Mbali na hilo Zamzama amedokeza kuwa kumekuwa na unyanyasaji kwa pesa ya walemavu ikiishia mikonono mwa watu.

Pia Zamzam amempongeza mwenyekiti wa mashirika hayo Zedekiah Adika  kwa kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za kibinadamu akimtaka Rais William Ruto kuangalia maswla ya walemavu akisema idadi yaoni ndogo mno na serikali  haiwezi kushindwa.

“Hii ni serikali ambayo inafaa kuangalia mnyonge vituv vyao ikiwemo misaada yao ije kwa wakati,afadhali watu wengine wakosa lakini walemavu wapate.”Akasema Zamzam.

Kiongozi huyo amerai viongozi wa marengo miwili kufanya mazungumzo ili kuleta amani katika taifa.

BY EDITORIAL DESK