GamingHabariMichezoNewsSports

MAMBO NI 3, Arsenal Yainyuka Man United 3-1 Ligi kuu Uingereza

Mchezaji wa safu ya kati Dencan Rice na Gabriel Jesus walifunga mabao katika dakika za lala salama na kuipelekea klabu ya Arsenal kuchukua ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Manchester United.

Klabu hizi mahasimu wa jadi zilipimana nguvu Septemba 3, 2023 katika uga wa Emirates Uingereza. Bao la Manchester likitiwa wavuni na mshambulizi matata Marcus Rashford dakika ya 27, bao lililokombololewa kupitia mkwaju wa kapteni Ordegard aliyemuacha mlinda lango Onana kuambulia patupu katika dakika ya 28.

Mwishoni mwa kipindi cha pili dakika ya 96 Sajili mpya Rice, aliokoa timu yake kwa kutikisa nyavu kupitia Kona Iliyosawazishwa na Bukayo Saka. Jesus katika dakika 11 za nyongeza ya kipindi cha pili, alizima matumaini ya mashetani wekundu kwa kufunga bao la kimataifa na kuipatia Arsenal ushindi wa bao 3.

Mkufunzi Mikel Arteta alisifia ushindi huo akiutaja kama ‘Nia Ya Kushinda’, kumbukumbu itakayosalia katika vichwa vya washika bunduki kwa muda mrefu.

Nyakati hizi zitashikamana nasi, na umati uliounganishwa kwa timu pamoja na historia kubwa ya mechi hizi, ni vyema sana. Nia, dhamira ya timu, ambayo itashinda na kwenda na kwenda mbele, ninajivunia kwao.” Alisema

Hata hivyo mkufunzi Erik ten Hag wa Manchester, alidai kuwa bao la Alejandro Garnacho kipindi cha pili lilipaswa kupitishwa akilaumu VAR kwa kukakataliwa kwa bao hilo; Ten Hag pia alihisi Man Utd walipaswa kupewa penalti na bao la dakika za mwisho la Declan Rice lilipaswa kukataliwa.