HabariNews

Madaktari Mombasa Waanza Mgomo licha ya Agizo la Mahakama Kuusitisha

Hatimaye Madaktari hapa kaunti ya Mombasa wameanza rasmi mgomo wao wakilalamikia masuala mbalimbali ya utekelezwaji wa maslahi na matakwa yao wanayoshinikiza.

Madaktari hao wanashirki mgomo huo wakilalamikia hatua ya serikali kwa kushindwa kuwapandisha vyeo licha ya kuhudumu kwa muda mrefu sawia na kukabiliana na uhaba wa madaktari kote nchini.

Aidha, wanailaumu serikali kwa kutoajiri madaktari wanagenzi wa nyanjani (medical interns) na kutoshughulikia lalama zao kuhusu bima mpya ya Afya ya Kijamii, SHIF.

“Sasa hivi tuna tatizo, Mombasa ina shida hiyo, Kilifi kaunti, Kaunti ya Lamu hali ndio mbaya kabisa, Tana River halkadhalika madaktari 26 pekee kaunti nzima. Ni aibu ilioje!”

Sasa hivi tumekuja mbele yenu kuiambia (serikali) haturudi nyuma, haturudi kazini tushaweka zana zetu chini, na zetu ni kila kitu, lakini kama mtu hataki kusikiliza kazi yetu ni kuondoa huduma kwa umma,” walisema.

Mgomo sawia na huo unafanyika huko kaunti ya Uasin Gishu ambako madaktari wamewashauri wagonjwa kusaka huduma za matibabu katika hospitali za kibinafsi.

Wameapa kutorejea kazini hadi pale maslahi na matakwa yao yatakaposhughulikiwa.

Ikumbukwe kuwa siku Jumatano Machi 13, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Leba Bryam Ongaya alikuwa ametoa maagizo kwa KMPDU kusitisha mgomo wao ili kutoa mwanya wa kupatikana suluhu dhidi ya mzozo huo.

Hii ni licha ya Katibu Mkuu wa KMPDU Davji Atella kusisitiza kuwa mgomo huo uliopangiwa kuanza saa sita usiku wa kuamkia Alhamisi kuendelea kama ulivyopangwa.

BY NEWS DESK