HabariNews

Walimu wa Sekondari Msingi (JSS) Kilifi Waandamana Kushinikiza Serikali iwape Mkataba wa Kudumu

Walimu wa Shule za Sekondari msingi JSS, kaunti ya Kilifi mnamo wameandamana kwa kile wanachodai kuwa kutopewa mikataba ya kudumu licha ya kufanya kazi kwa zaidi ya ule muda unaohitajika ili kuajiriwa rasmi.

Walimu hao wanagenzi wameapa kususia kazi na kutorejea shuleni punde zikapofunguliwa iwapo Serikali haitawaajiri rasmi kwa mkataba wa kudumu na marupurupu mengine sawia na kuwafidia kwa muda waliohudumu.

Kulingana na Joseph Moseti mmoja wa walimu ni kuwa kutoajiriwa kwa mkataba wa kudumu kunazidi kuwafanya walimu kupitia hali ngumu za kimaisha, tofauti na wafanya kazi wengine.

Walimu hao wameapa kutolegeza msimamo wao, huku wakieleza kuwa hawatarudi kazini mpaka lalama zao zisuluhishwe.

“Tunaimbia TSC tumechoka na hutaendelea kujiita wanagenzi kwa sababu sisi si walimu wanagenzi tena, mahakama ilitoa uamuzi wake na huu ni mwanzo tu wa maandamano hatutaruhusu mwalimu yeyote aendelee kuteswa Kenya hii, kwanza suala la uanagenzi kwa walimu si halali kisheria lazima waandike walimu na watufidie.” Alisema

Aidha wametoa makataa ya siku saba kwa tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC kuelezea umma iwapo ni nani anayehusika kwenye swala la uajiri wa walimu huku wakiwataka wabunge kukoma kuingilia maswala ya uajiri wa walimu nchini.

“TSC tunawapa makataa ya siku 7 mtuambie na mzungumze kwa umma kwamba ni nyinyi mnaopaswa kuajiri walimu au ni wabunge. Punda amechoka!”

Wameongeza kuwa mapendekezo yaliyotolewa na wabunge yanalenga kukiuka haki za walimu na kuwakandamiza.

BY ERICKSON KADZEHA