Hatimaye Rais William Ruto amemteua Dorcas Oduor kuchukua nafasi ya Mwanasheria Mkuu nchini.
Oduor ambaye kwa sasa anafanya kazi katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kama katibu mkuu, ni wakili wa Mahakama Kuu nchini.
Ana shahada ya uzamili katika kitengo cha usimamizi wa migogoro ya kimataifa kutoka chuo kikuu cha Nairobi pamoja na shahada ya uanasheria kutoka chuo hicho.
Kulingana na taarifa ya Rais ni kwamba Dorcas Oduor ni mchapakazi na mwenye uadilifu na endapo bunge la kitaifa litampiga msasa na kumuidhinisha basi atakuwa mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa wa mshauri mkuu nchini.
Haya yanajiri baada ya rais Ruto kuvunjilia mbali baraza lake akiwemo mwanasheria Mkuu Justin Muturi na kuanza kulipanga upya.
BY EDITORIAL DESK