MichezoSports

Saldido Mshindi wa 500,000 Shindano la Tujiamini na SportPesa 2024 Ukanda wa Pwani

Leon ‘Saldido’ Nzaro ndiye mshindi wa shilingi laki tano katika shindano la Tujiamini na SportPesa la mwaka 2024 ukanda wa Pwani.

Mshindi huyo wa mashindano ya baiskeli ya mwaka wa 2023 zilizoandaliwa Katika Kaunti ya Kilifi mnamo mwezi Aprili 2023 aidha aliwashukuru wadau wote waliofaniukisha azima na ari yake ya kutamba katika mbio hizo za baiskeli.

Akizungumza Katika hafla iliyoandaliwa Ijumaa Novemba 29 mjini Mombasa ya kumtangaza rasmi mshindi wa shindano hilo, Leon ameishuruku kampuni ya SportPesa kwa jitihada zake katika kutambua na kukuza vipaji akisema tuzo lake litamfaa pakubwa katika maandalizi ya mashindano yajayo ya Kimataifa.

“Kwanza ninashukuru kwa tuzo hili na kwa kweli Tujiamini itanisaidia kujisajili katika mashindano ya mwakani na kununua vijaa vya kisasa vya kutumia katika mazoezi yangu. Kwa sasa nitandelea kufanya mazoezi yangu nikilenga mashindano ya olimpiki na mashindano mengine ya kimataifa.” Alisema Leon

Kwa upande wake Abdulaziz Mubarak ambaye ni kocha mkuu wake Leon alisifia juhudi za mwanafunzi wake akimtaka azidishe juhudi zake lengo kuu likiwa ni kushiriki mashindano yajayo ya kimataifa hapo mwakani.

Mubarak kadhalika alihimiza haja ya vijana wenye vipaji kupalilia talanta zao kwa kufanya mazoezi zaidi ili kutimiza malengo na azima zao maishani.

“Nina furaha sana kwa Leon kushinda tuzo hili na ninamuhimiza aendeleza juhudi zake ili afikie malengo yake. kwa sasa anatakiwa kuwa mwenye ujasiri na kujiamini anapojiandaa kushiriki majaribio ya kitaifa ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani.Tunashuru kwa fursa hii na tuna matumaini ataendelea kujikuza na kuboresha kipaji chake kila uchao.” Alisema Abdulaziz.

Kwa upande wao wadhamini wa shindano la mwaka huu la tujiamini na SportPesa wakiongozwa na afisa mkuu wa masuala ya ushirikiano katika kampuni hiyo Willis Ojwang alisema wataeleza juhudi za kutambua na kukuza vipaji kote nchini.

Aidha afisa huyo aliwataka wahisani na wafadhili wengine kujitokeza na kushiriki katika kunoa vipaji mijini na vijijini akisema hii ni mojawapo ya njia ya kuhakikisha vijana wanatambua talanta zao na kuzitumia kujikimu ki maisha.

“Tujiamini imefika sehemu nyingi nchini na imeweza kutambua vipaji katika sehemu ambazo hazimna umaarufu wa kukuza vipaji. Nawamiza washirika wengine kuwekeza katika kukuza vipaji vya vijana na kuwasaidia ili kuafikia ndoto na azma zao.Tutandeleza mchakato huu kote nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi.” Alisema Willis

Baada ya hafla ya Kumtangaza mshindi wa mwaka huu ukanda wa pwani, sasa mchakato wa kutambua na kunoa vipaji zaidi katika ulingo wa soka ukanda wa Pwani unaendelae ambapo siku ya Jumamosi Novemba 30, Michuano ya Cheza Dimba na SportPesa inayojumuisha timu sita kutoka ukanda huu itang’oa nanga rasmi.

BY ISAIAH MUTHENGI