Habari

JAMII HUKO KWALE ZATAKIWA KUFAHAMU UMUHIMU WA KUELIMISHA WATOTO

Wito umetolewa kwa jamii Katika Kaunti ya Kwale kufahamu umuhimu wa kuwaelimisha watoto kuhusiana na haki zao za kimsingi na vile vile masuala dhulma za kinjisia.

Kulingana na Mshirikishi katika shirika la kijamii la Samba Sports Youth Agenda Nancy Wambura ni kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watoto na kuwa yatawawezesha kufanya maamuzi yatakayowasaidia maishani .

Wakati uo huo Wambura amesema shirika hilo limetoa mafunzo kwa wanafunzi wakike na wakiume zaidi ya 30 kutoka shule za msingi sehemu hiyo hatua inayolenga kuwanufaisha .

Aidha Wambura amesema badhi ya mada walizozipatia kipaumbele ni dhulma za kijinsia , na vipi mtoto anaweza kuchukua hatua kwa kupiga ripoti endapo atakumbana na visa vya kudhulumiwa .