Habari

Wakaazi Mwangulu KWALE walalamikia ongezeko la wanaume kujamiiana wao kwa wao

Baadhi ya wakaazi wa Kijiji cha Mwangulu kaunti ya Kwale wamelalamikia ongezeko la tabia ya wanaume kutendeana tendo la ndoa wenyewe kwa wenyewe.

Wakiongozwa na Mohammed Mwakuyala wakaazi hao wamesema vitendo vya uchafu huo vimekithiri pakubwa kuwafanya wanawakwe kuwa wapweke.

Wakaazi hao sasa wameilani tabia hiyo wakiwataka wanaume wanaondesha biashara hiyo kukoma.

Hata hivyo wakaazi hao wameonyesha hofu ya kwamba tabia hiyo huenda ikaathiri vijana wadogo na kizazi kijacho.

Aidha wameomba idara mbali mbali za kiserikali kuingilia kati na kuwachukulia hatua za kisheria kwa wanaokiuka maadili.