Habari

EACC yawataka wawakilishi wadi kuwajibika

Tume ya maadili na kupambana na ufisad EACC imewataka wawakilishi wadi nchini kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao.

Mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukala amesema visa ambavyo vimeshuhudiwa katika baadhi ya mabunge ya kaunti nchini ni vya kutia aibu.

Amesema kufikia sasa wanachunguza mabunge takriban 10 ya kaunti, kufuatia visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wawakilishi wadi wanapokuwa kazini.

Kaunti ya Baringo ni miongoni mwa kaunti zinazochunguzwa na EACC baada ya vurugu kushuhudiwa wakati wa kujadili mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.

Wakati huo huo amesema EACC inaendelea kukabiliana na vita dhidi ya ufisadi licha ya changamoto za uhaba wa fedha wanazokabiliwa nazo.