AfyaHabari

Chanjo ya COVID 19 yaanza kutolewa….

Kaimu mkurugenzi wa afya dkt Patrick Amoth ndiye afisaa wa kwanza wa umma kudungwa chanjo dhidi ya virusi vya corona inayojulikana kama Astra- Zeneca katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi.

Amoth amekuwa wa kwanza kupewa chanjo hiyo katika hospitali ya Kenyatta baada ya zoezi la kutolewa chanjo hiyo kuzinduliwa rasmi hii leo, huku afisaa mkuu mtendaji katika hospitali hiyo dkt Evans Makori akiwa wa pili kudungwa.

Wawili hao ni miongoni mwa wahudumu wa afya 10, ambao wamechanjwa hii leo kabla ya zoezi hilo kuanza rasmi jumatatu wik ijayo katika kaunti zote humu nchini.

Kabla ya kuchanjwa Amoth aliwahakikishia wahudumu wa afya kwamba chanjo jiyo ni salama.

Haya yanajiri huku hospitali zote za rufaa nchini zikipokezwa dozi za chanjo hiyo.

Katibu katika wizara ya afya DKT Susan Mochache anasema kaunti ya Nairobi ndio imepokea idadi kubwa ya chanjo hiyo kwa kupata dozi elfu 138 kati ya dozi elfu 495 zilizosambazwa kote nchini.

Kaunti ya Mombasa inatarajiwa kupokea chanjo elfu 54, Kilifi elfu 42, huku Dozi 60,000 zimesambazwa katika kaunti za kaskazini mwa bonde la ufa miongoni mwa kaunti nyingine.