HabariSiasa

Viongozi wa ODM Kwale wapinga chama kipya cha PWANI…

Viongozi wa chama cha ODM katika eneo la Pwani wamepinga vikali mpango wa kubuniwa kwa chama kimoja cha eneo hilo.

Mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kwale Zulekha Hassan amepuzilia mbali mpango huo unaosukumwa na gavana wa Kilifi Amason Kingi.

Kauli yake imeungwa mkono na Seneta wa kaunti hiyo Issa Boi anayewataka viongozi wa Pwani kukiunga chama cha ODM.

Kwa upande wake mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga amesema kuwa wakaazi wa Pwani wataunganishwa kupitia chama cha ODM.

Chonga amewataka viongozi wa Pwani kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga kufuatia ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta.