Habari

Tume ya kitaifa ya uwinao na utangamano NCIC itachukua hatua kali dhidi ya viongozi wanaowachochea Wakenya kukutekeleza uhalifu .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi hii leo , mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Samuel Kobia ameonya kuwa viongozi watakaopatikana na hatia hiyo watazuiwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kobia ameitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuingilia kati kuona kuwa sheria hiyo itafuatwa ili Kenya iwe nchi yenye amani na utulivu.

Ameyasema hayo akisitiza kuwa tume yake pamoja na EACC , zitafuatwa ushauri wa mahakama kuona kuwa viongozi wanakuwa na nidhamu na maadili ya kudumisha usalama.