AfyaHabariLifestyleWorld

Mshirikishi wa watu wanaoishi na ulemavu …

Bi Zaja anasema wakenya wanafaa kuhamasishwa zaidi kuhusu chanjo hiyo kutokana na dhana zinazoenezwa kuhusu chanjo hiyo.

Katika mahojiano na Sauti ya Pwani Fm, Bi Zaja amesema propaganda zinazosambazwa sehemu mbali mbali ikiwepo kwenye mitandao ya kijamii huenda zikachangia wakenya kukosa imani na chanjo hiyo.

Wakati huo huo ameitaka serikali kutoa chanjo hiyo bila malipo kwa wakenya, akisema huenda wengi wanaohitajika kupokea chanjo hiyo wakokosa uwezo wa kuigharamikia.