Habari

KAUNTI YA KILIFI YAKOSOLEWA KWA UTEPETEVU.

Aliyekuwa mgombea kiti cha Ubunge mjini Malindi Phillip Charo sasa anaitaka Serikali ya Kaunti ya Kilifi kujitokeza na kueleza utepetevu katika idara ya maswala ya dharura mjini humo.

Hii Ni baada ya Hoteli ya Oasis Village mjini humo kuteketea moto hapo jana na kusababisha hasara kubwa ya mali.

Charo amedai kwa muda sasa mali ya Mamilioni ya fedha imekuwa ikiteketea bila kupata usaidizi kutoka kwa vitengo husika vya Serikali ya Kaunti, akisema kuna haja ya wenyeji kupata maelezo zaidi kuhusu utepetevu huo.

Wakaazi walioshuhudia mkasa huo wamedai utepetevu katika vitengo cha wahudumu wa zima moto umepelekea mali hiyo kuteketeza.

Wanadai magari ya zima moto yangefika kwa wakati mali iliyoteketea ingeokolewa japo hakuna kisa chochote cha maafa kilichoripotiwa.