AfyaHabari

Serikali yaombwa kulipia wazee bima ya NHIF.

Serikali ya kitaifa imeombwa kuwalipia bima ya kitaifa ya afya NHIF wazee ambao wanapokea pesa za mpango wa inua jamii.

Kulingana na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire serikali ya kitaifa ina mpango wa kuwalipia wazee bima hiyo ambayo anasistiza kuwa itawasaidia wazee hao kugharamia malipo ya magongwa mbalimbali yakiwemo shikinikizo la damu ,saratani na menginenyo.

Mwambire amesema usajili  wa wazee hao  utaanza hivi karibuni ili waweze kuingizwa kwa mpango huo wa kulipiwa bima ya afya kila mwezi.

Aidha Mwambire amewataka wazee ambao wanapokea pesa za mpango inua jamii kutenga shilingi 500 ili kujipilia bima hiyo ya afya.

By Erickson kadzeha