AfyaHabariWorld

WAKAAZI KWALE WAOMBWA KUFUATA SHERIA ZA COVID 19

Waziri wa afya kaunti ya Kwale Francis Gwama ameonya wakaazi dhidi ya kutofuata maagizo ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona baada ya uzinduzi wa zoezi la kutoa chanjo ya corona.

Gwama amewahimiza wenyeji kuendelea kuvaa barakoa na kunawa mikono ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona.

Waziri huyo amedokeza kwamba takriban watu 500 wamethibitishwa kuambukizwa corona tangu kuripotiwa kisa cha kwanza kaunti hiyo.

Vile vile amebainisha kuwa wagonjwa wa corona waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Msambweni wamepona ugonjwa huo.