HabariLifestyleTravel

Huenda Mabadiliko yakafanyika katika sekta ya uchukuzi wa umma hasa kuhusu idadi ya abiria wanaobebwa kwenye magari ya umma.

Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali Cyrus Oguna  aliyekuwa akizungumza na wanahabari wa hapa Mombasa.

Oguna ametetea  hatua ya serikali kuendeleza uchunguzi wa abiria wanaotumia SGR hadi nyakati za usiku  na kukosa kueka umbali  unaohitajika ili kudhibiti maambukizi ya corona

Oguna ameshikilia kwamba ni jukumu la kila mwananchi kukataa kuabiri magari ya umma yasiyozingatia sheria zilizowekwa ili kujiepusha na athari za kuambukizwa ugonjwa huo  ambao umeibuka upya .

Oguna aidha ametoa ushauri kwa washika dau katika sekta ya utalii pwani kufanya kila juhudi kuboresha utalii na kuongeza kua serikali imejizatiti kwa kubuni hazina maalum  ya kuwasaidia wamiliki wa hoteli waliofilisika kutokana na janga la corona na kuanza upya.