HabariKimataifa

Ibada ya kuombea na kuaga mwili ya mwendazake aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli inaendelea kwa sasa katika kanisa la St Peters jijini Daresalaam.

JOHN POMBE MAGUFULI

Ma mia ya waombolezaji  wakiongozwa na Rais wa  Tanzania Samia Suluhu Hassan wameweza kufika katika kanisa hilo kuuaga mwili wa hayati Magufuli.

Aidha viongozi huku Kenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wanatia sahihi katika kitabu cha kutoa risala za rambirambi za hayati Magufuli.

Baada ya ibada mwili wake mwendazake utapelekwa katika uwanja wa Uhuru kuagwa na viongozi na kesho kusafirishwa kuelekea Dodoma ambapo utaagwa rasmi.