HabariSiasa

Ruto asema anaweza kufanya kazi na Raila kaba ya uchaguzi mkuu……

Naibu rais William Ruto sasa anadai kwamba yeye na kinara wa ODM Raila Odinga ndio viongozi pekee wanaoamini katika mtizamo wa chama cha kitaifa.

akihojiwa na kituo kimoja cha radio humu nchini, Ruto amesema hakuna kinachowazuia yeye na Raila kushirikiana kisiasa.

Ruto alikuwa akizungumzia hatua ya viongozi mbali mbali nchini kuungana kwa ajili ya siasa za mwaka 2022 akisema hatua hiyo huenda ikaligawanya taifa hili kwa misingi ya ukabila.

amesema miungano inayobuniwa inapaswa kuwa na sura ya kitaifa ili kuwaunganisha wakenya badala ya kuunganisha watu wa maeneo Fulani pekee.

Wakati huo huo Ruto ametetea siasa za hasla nation akisema zinalenga kuwaunganisha wakenya wote na wala hazina lengo la kuwagawanya wakenya kwa misingi ya walivyonavyo na wasiokuwa navyo akisema siasa za hasla zinawashirikisha wakenya wote wanaolenga kujiimarisha kiuchumi.