HabariKimataifa

Hatimaye hayati Magufuli azikwa huko kwao Chato….

Aliyekuwa rais wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli amezikwa alasiri ya leo kwenye makaburi ya familia nyumbani kwao Chato–Kagera nchini Tanzania.

Akihutubia waombolezaji  kwenye hafla ya mazishi ya  mwendazake katika eneo la chato, Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kutekeleza miradi yote ambayo iliachwa bila ya kutekelezwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo hayati Magufuli.

Rais Suluhu amesema kwamba miradi yote iliyowachwa bila kukamilika itakamilishwa pamoja na kutekeleza ahadi ambazo mwendazake alizoziacha kwa  watanzania huku akiwataka watanzania kushirikiana.

Vile vile Suluhu amewapongeza wale wote waliohusika kwa hali na mali kuona kwamba wanafanikisha safari ya mwisho ya kiongozi huyo, kauli iliyoungwa mkono na waziri mkuu wa Tanzani Kassim Majaliwa.

Magufuli aliaga dunia mnamo machi 17, kwenye hospitali ya Mzena alipokuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa moyo.